Jumamosi 27 Septemba 2025 - 06:55
Mfalme wa Hispania azitaja hatua za Israel kuwa “za kuchukiza na kinyume na dhamiri ya kibinadamu”

Hawza/ Felipe wa Sita, Mfalme wa Uhispania, katika hotuba yake kwenye Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa, akizungumza kwa msimamo mkali dhidi ya hatua za utawala wa Kizayuni huko Ghaza, alitoa wito wa kusitishwa mara moja kwa mauaji ya raia wa Kipalestina.

Kwa mujibu wa kitengo cha tarjama cha  Shirika la Habari la Hawza, Mfalme wa Uhispania, katika hotuba iliyodumu kwa dakika 20, akiwa katika mkinzano wa wazi na mitazamo ya Donald Trump, Rais wa Marekani, na pia mitazamo ya mirengo ya kulia nchini Uhispania ikiwemo Chama cha Watu (Partido Popular) na Chama cha Vox, vilikosoa vikali msimamo wa serikali ya Israel.

Felipe wa Sita, sambamba na hayo, alisisitiza kwamba Israel inapaswa bila sharti lolote kushikamana na sheria za kimataifa za kibinadamu kote Ghaza na Ukingo wa Magharibi, aidha, alitetea kitendo cha Uhispania na wanachama wengine wa Umoja wa Mataifa kulitambua taifa la Palestina.

Vilevile, alitaka uungaji mkono Umoja wa Mataifa kama mdhamini wa maadili ya pamoja ya kibinadamu, na akijibu mtazamo wa dharau wa Trump kuhusu taasisi hii, alisema:

“Kuwa na imani na Umoja wa Mataifa kunamaanisha kuwa na imani na ulimwengu unaoongozwa na sheria na kanuni; ulimwengu ambao ndani yake heshima ya kibinadamu haiwezi kujadiliwa.”

Mfalme wa Uhispania katika sehemu nyingine ya hotuba yake alihoji sera za kupinga uhamiaji za mirengo ya siasa kali, na akautaja uhamiaji kuwa ni “chombo cha maendeleo ya pande zote ambacho kinapaswa kusimamiwa kwa misingi ya haki za binadamu. Pia alisisitiza juu ya ulazima wa kukabiliana na mgogoro wa tabianchi, uchafuzi na uharibifu wa urari wa viumbe hai, na alitoa wito wa kuharakishwa kwa mchakato wa mpito wa haki kuelekea kwenye nishati jadidifu.

Kwa jumla, hotuba hii ilikuwa ni kielelezo cha mtazamo ulio kinyume kabisa na misimamo ya Trump na mirengo mingi ya mrengo wa kulia, ndani na nje ya Uhispania, japokuwa Felipe wa Sita, katika kuchagua misemo yake, aliepuka kutumia neno “mauaji ya halaiki (genocide).”

Lebo

Maoni yako

You are replying to: .
captcha